Tuesday, December 22, 2009

mwimbaji lady issa aomba msaada,yuko mahututi.

LADY ISSA wakati wa harusi yake (kutoka hana uwezo wakulipia matibabu "Lady Issa" Hospitalini amefukuzwa) (Mwanamziki wa Kike ambaye alijinyakulia sifa katika miaka ya 80 kabla yakuokoka nakuimba Nyimbo za Injili katika Mwaka wa 2000,sasa hivi ni mahututi Mjini Kinshasa) (Tarehe 11.12.2009 Saa 5 na nusu majira ya Kinshasa Lady Issa kapiga simu gazetini kalazimika kuondoka katika hospitali ya kijeshi "Kokolo" na kuachia maisha yake katika mikono ya Mwenyezi Mungu. (Mratibu wa Chama chakusaidia Wasanii Tshaka Kongo aomba msaada ili Lady Issa achangiwe pesa apate matibabu). Kingunza Kikim Afri

The Ngoma Africa band! inawatakia X-Mass njema na heri ya mwaka mpya

Watumishi wenu "The Ngoma Africa band" aka FFU inawatakia wadau wote wa Bambataa ! X-Mass Njema na heri ya mwaka mpya 2010, Malikia pia usikose kutumulikia taa aka "Bambataa" hili mwaka 2010 tuone mbali

Sauti za Busara 2009 Music Festival.

The seventh edition of the Sauti za Busara music festival will take place in Zanzibar, 11-16 February 2010; admission is free to all EA Residents before 5pm. Sauti za Busara (Sounds of Wisdom) is an international festival celebrating East African music taking place around the second weekend of February each year in Zanzibar. Proudly sponsored by Zantel. how to get there? where to stay? The Festival Finalé Party is on Tuesday 16 February 2010 from 4pm - 4am at a beautiful beach location in Jambiani, on Zanzibar's east coast. For bookings across a range of hotels in Jambiani (prices $30 - $130 per room) and for information about transport from Stone Town please contact: info@zanzibarhotelgroup.com or +255 777 504 044 or +255 785 099 263

The Best of Msondo Ngoma Band

Hakuna mashaka yoyote unapozungumzia habari za mziki wa dansi nchini,uwezi kukosa tugusia bendi kongwe "Msondo Ngoma Band" aka baba ya mziki, wazee wa mambo hadharani.Pia utakubaliana na mimi kuwa Msondo Ngoma band ina haki ya kujigamba katika kila hali kuwa ndiye baba wa mziki,na ndio bendi pekee iliyomudu misuko suko na mawimbi ya kila aina katika gemu la mziki wa dansi! kama utakubali au la! bendi hii maarufu hapa nyumbani ndio bendi pekee kongwe ya mziki wa dansi barani Afrika,kutokana na utafiti unavyoonyesha,msondo ilizaliwa 1964 kama Nuta jazz ilikuwa inamilikiwa na umoja wa wafanyakazi(NUTA),baadae JUWATA na sasa inajitegemea,Bendi hii maarufu ina CD "Best of Msondo Ngoma" ambayo inapatikana katika maduka ya STRENE Music mjini London,Uingereza aka kwa bi.mkubwa Ukerewe,CD hiyo pia inapatikana katika maduka mbali mbali ya ughaibuni,juhudi za kuitangaza CD hiyo zimefanywa na "Ujamaa Record" ya Uingereza,kwa moyo wao wa kizalendo "Ujamaa Record" wamefanya kitendo ambacho washabiki na wapenzi wa dansi la bongo,wanaweza kuinunua CD hiyo na kujivunia kuwa Tanzania ina "baba ya mziki", ambayo tena ni bendi kongwe kuliko zote barani Afrika! kongwe kwa sababu bendi zote zilizozaliwa umri sawa na "Msondo Ngoma" kwenye miaka ya 60s hazipo tena, yaani marehemu!zimekufa,tulikuwa tunasema kuwa bendi kongwe ni TPOK Jazz iliyoanzishwa mwaka 1956 ya marehem Franko Rwambo Makiadi,nayo alipokufa Franko,bendi ikajibadili jina kutoka OK na kuitwa Bana OK! ndio kimoja.ilijikongoja lakini wapi?bendi kongwe ingine kule Kinshasa ni "Zaiko langa langa" lakini Msondo Ngoma bado kongwe kwani ina umri mrefu kuliko zaiko,na kama tukienda kule Senegar kuna watu wazima wa bendi ya Baobab Band lakini bendi hiyo ilianzishwa miaka 1970s,Msondo Ngoma bado babu yao! hata bendi maarufu ya mziki wa Salsa, AFRICANDO ambayo inawanamziki mchanganyiko kutoka karebian na Afrika magharibi,haiwezi kufikia umri wa Msondo Ngoma band babu yao! kwani bendi ya Africando ilianzishwa miaka ya 1970 na kina marehemu Peppy Seck wa Senegar,wakiwamo akina Bonkana Maiga.Lakini sasa umri sio hoja bali matunda yepi tunavuna au tumeyavuna ?hili ndilo swali linalotakiwa kujiuliza,mbona wenzetu wanamejitangaza kwa wingi nje ya nchi na kuvuna walichokivuna! na kila mwaka wanapiga Tour za kimataifa! sisi tumekosea mahala gani?tufanye nini ? hili nasi tuwe kama wenzetu? Labda wadau na watanzania wenzetu mlio nje ya nchi je ! labda tungewaomba tufanye "Harambe la pamoja" hili tuzitoe nje bendi zetu nasi tuwe kama wenzetu,ndio tuseme hili haliwekani au? Najua penye nia pana njia wwe na mimi,sisi na nyinyi tunaweza kuufanya huu mziki wa Tanzania ukawa wa kimataifa,bendi zetu zinahitaji msaada na mchango wenu,promotion na kadhalika na hayo yote hayawezi kufanywa na wana mziki bali mimi na wewe,au sisi na wewe. Ni mimi Malikia wako Sophia Kessy katika kukuza na kuendeleza sanaa na mziki,usikose kunitumia barua pepe kama unaushauri kwa nyie wenzetu milio nje ya nchi na ndani pia.Nimalizie makala hii kwa wito wa vionjo vya msondo "Kidogo tu! Kidogo tu! haya twendeee!!!!!

Show ya mama Tshala Muana ilivyofana

MJ 3O BINTI HUYU NI HATARI KWA KUIMBA NI MWIMBAJI WA MAMA TSHALA MUANA NA NIKIZAZI KIPYA CHA DANCE MMOJA KATI YA WAIMBAJI NINAO WAHUSUDU KUTOKA KONGO PAMOJA WENGINE TOKA HAPA NYUMBANI KAMA JD NA WENGINE KIBAO TU WANAVYO NIKOSHA
mie na mama Tchala muana jamani ukweli ni kuwa mama huyu sasa ni mkubwa sana ila kazi ilionekana
mie na kaka G kaptain wa jahali la Clouds tulikutana pia jijini
mie ni miongoni mwa wadau ambao nilipata nafasi ya kushuhudia show ya mama Tshala Muana mapema jana tu pale Jijini Arusha katika pita pita zangu za kumalizia kajilikizo basi kwa bahati nzuri hoteli niliofikia ndipo ilipopigwa show ya mwana mama huyu jemedari na nguli katika muziki na miondoko ya Mutwashi ukweli ni kuwa kwa mujibu wa wadau walioshuhudia show ya Mama Tashala Muana ya Dar Es Salaam na na ile iliopigwa pale Naura spring Hotel Arusha wadau wanasema ya Arusha ilifana sana ingawa hakukuwa na watu wengi show ilikuwa ni ya kistaarabu ya utulivu na raha ya kutosha naomba kuwasilisha baadhi ya picha za maukio ya show hiyo BURUDANI ILIKUWA SI MCHEZO
UNA BISHAAAAAAAAAAAAAAAAA MMH BIBIE YUPO KAZINI MAMA YA LONDON
MAMA TSHALA MUANA AKIFANYA KAZI
burudani inapokolea mwe mwe mwe mwe jamani nimekumisssssssssssssssss

Mwanamziki Ras Nas na CDs yake "Dar es salam,kutoka Norway

Bila shaka ushawahi kumsikia mwanamziki Nasibu Mwanukuzi aka Ras Nas anayefanyia shughuli zake nchini Norway, Ras Nas,ni moja wa wanamziki ambao wameitangaza vema Tanzania ughaibuni,mwanamziki huyu msomi mwenye shahada ya sheria kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam,pia shahada zingine kutoka vyuo mbali mbali vya ughaibuni,linapokuja swala la uzalendo na utamaduni Ras Nas usomi wake anauweka pembembeni na kupanda jukwaani kuipeperusha bendera ya bongo kwa njia ya mziki.Kwa ufupi tu historia ya Ras Nas katika ulingo wa mziki,inaanza toka alipokuwa mvulana kwani mziki wa "Sekuse kilikili" la marehem Mbaraka Mwishehe na Morogoro Jazz ndio kikoo au taa iliyomuamasisha Nasibu Mwanukuzi aka Ras Nas kufikia halipo. Miaka ya 1980s Ras Nas na wenziwe walianzisha Kikundi cha sanaa za maonyesho mjini Dar, kilichojulikana kama "SAYARI NGOMA TROUPE" katika kikundi iko kulikuwapo Mwanadada Chiku Ali,Fredy Macha,George Chioko na Ras Nas.tuseme kilikuwa ni kukundi cha wasanii wasomi kwani wengi wao walitokea Chuo kikuu cha Dar (UDSM) na kuhuweka usomi wao pembeni nakuliendeleza libeneke la sanaa. RAS NAS ni mtunzi,mwimbaji na mshahiri na mpiga gitaa !sasa anatamba na CD yake iliyobeba jina la "Dar-Es-Salaam" msikilize Ras Nas katika www.myspace.com/ras_nas

Sunday, December 20, 2009

NAOMBA RADHI WADAU WANGU

NAWAOMBA WADAU WANGU KUTOKANA NA SABABU ZILIZOKUWA NJE YA UWEZO WANGU WADAU SIKUWEZA KUWA NANYI BEGA KWA BEGA KATIKA KUENDELEZA GURUDUMU LETU LA BURUDANI NAJUA MATUKIO MENGI SANA YAMEPITA NA HUKUWEZA KUPATA TAARIFA NAOMBA KUCHUKUA FURSA HII KUWATAKA MNIWIE RADHI NA KUELEWA KUWA KUANZIA SASA TUTA ENDELEA KUWA PAMOJA HIYO NI AHADI YANGU KWENU. NILIKUWA NJE YA MKOA NA MIKOA SO MAENDEO AMBAYO NILIKUWA KWA MUDA WA WIKI NZIMA HAKUKUWA NA MAWASILIANO YA NAMNA YOYOTE ILE ELEWA KUWA HII NI TANZANIA NA KUNA MAENEO HUDUMA NYETI KAMA INTERNENT ZINAKOSEKANA KABISA MSIJALI AM BACK AGAIN ONE LOVE. SOPHIA KESSY MALKIA WENU

Friday, December 11, 2009

mie ndio huyu ulie omba picha

malkia wako
kuna mdau ameomba kuniona leo haya huyu ndie malkia wa bambataa hope utakuwa umefurahi ... usikose kupitia pia blog mama ya ................http://malkiawako.blogspot.com/ kuna mengi ambayo utayapenda